Mnyama
Ufunuo 13: 14-18 "Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yeke. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza ambaye jeraha lake la mauti lilipona.Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya mot kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyai sanamu yule mnyama aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia punzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauwawe. Naye awafanya wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao, tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita."
Kumtambua Mnyama
Kabla hatujazugumza kuhusu mnyama ni lazima tujue Umbele na historia iliyokuwako kabla ya mnyama.Mahali pazuri kuanzia ni katika kitabu cha Danieli ,ambacho kina husika na unabii ,kuanzia karne ya 6 kabla kuzaliwa Kristo kuendelea hadi mwisho wa wakati.
Kuelezea mifano iliyotumiwa katika unabii wa Biblia haijawachwa kwa mwadamu kubahatisha tu .
Unabii ni Historia iliyotangulia kuandikwa kabla,na kitabu cha Danieli kinatoa funguo za kuielewa vizuri .Mnyama katika unabii inashiria Mfalme au Ufalme ."____ Ufunuo 13:14-18 "Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene,na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao, tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnayma yule, au hesabu ya jina lake.Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita." Danieli 7:17 Wanyama hao wakubwa walio wane ni wafalme wane watakaotokea duniani. Danieli 7:23 Danieli 7:23 Akanena hivi Huyo mnyama wa nne atakuwa ni mfalme wa nne juu ya dunia, atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga na kuivunja vipande vipande.inayoenyesha hii .Tazama ya kwamba "Mfalme" na "Ufalme" inatumiwa kwa usawa. Danieli 7:23 Akanena hivi Huyo mnyama wa nne atakuwa ni mfalme wa nne juu ya dunia, atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga na kuivunja vipande vipande. inaeleza ya kwamba hawa wafalme wanne "walitoka ndani ya bahari "na bahari na maji mengi" katika unabii hufananishwa na "watu ,na mkusanyiko na taifa na lugha "Ufunuo 17:15 . "Kisha akaniambia yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba ni jamaa na makutano na mataifa na lugha" . Katika Danieli 7 tunayo mambo ya sasa ,na ya baadaye ya falme za ulimwengu alizoonyeshwa nabii .
![]()
Mnyama kama Simba
Danieli 7:4 Wa kwanza alikuwa kama Simba naye alikuwa na mabawa ya tai nikatazana hata mabawa yake yakafutuka manyoya akainuliwa katika nchi akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Hii inahusu utawala wa Kibabeli ,iliyotawala hasa wakati wa akina Danieli
Mnyama kama Dubu
Danieli 7:5 Na tazama mnyama mwingine wa pili kama dubu naye aliinuliwa upande mmoja na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake. Wakamwambia ,nyama huyo hivi inuka ule nyama tele. Ishara hii ni sawa na ile inayopatikana katika Danieli 2:39 "Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine wa tatu wa shaba utakaoitawala dunia yote."
Ufalme uliyo fuata Babeli ni wa Waamedi na Waajemi .Hii ilikuwa utawala mara mbili ikiwa na Waamedi wakitawala kwanza ,kisha baadaye Waajemi .Unabii unaonyesha hili kwa kuonyesha ya kwamba Dubu "alijiinua pekee upande mmoja ".Mbavu tatu inawakilisha nguvu ambazo iliangusha ilipokuwa inainuka ,hii ikiwa LYDIA ,Baylon na Misri .
Mnyama kama Chui
Danieli 7:6 Kisha nikatazama na kumbe! Mnyama mwingine kama chui naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne akapewa mamlaka. Mfano huu unawakilisha utawala sawa na ule unaoonyeshwa katika Daniel 2:39. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishida na kama vile ilivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine wa tatu wa shaba utakaoitawala dunia yote.
Hii ilikuwa utawala wa Ugiriki chini ya Alexander Mkuu ambayo iliwapindua Waajemi ,na alipokufa utawala wake ukagawanyika katika sehemu nne ,kama mfano unavyoonyeshwa na vichwa vinne .
Mnyama wa nne
Danieli 7:7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku na tazama mnyama wa nne mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi naye alikuwa na meno ya chuma makubwa sana alikula na kuvunja vipande vipande na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake na umbo lake lilikuwa mbali sana na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Danieli 2:40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishida na kama vile ilivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
"Baadaye nikaona katika njozi ya usiku na tazama mnyama wa nne mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi naye alikuwa na meno ya chuma makubwa sana alikula alikula na kuvunja vipande vipande na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake na umbo lake lilikuwa mbali sana na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi "
Mfano huu pia ni nguvu sawa na ile inayoonyeshwa katika Danieli 2:40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishida na kama vile ilivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
Utawala wa nne utakao tawala kote duniani baada ya siku za Danieli ni Rumi ya Kishenzi .Ilikuwa tofauti na wanyama wegine ambao Danieli aliwajua hata akashindwa kuipa jina .Haingeelezeka .Pembe kumi imeonyeshwa katika
Danieli 7:24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao naye atakuwa mbali na hao wa kwanza naye atawashusha wafalme watatu.kama "Wafalme kumi watakao inuka ".Ni jambo la kweli ya kwamba utawala wa Kirumi uligawanyika tawala ndogo kumi kati ya mwaka 351 na 476 A.D.
Majina yao ya zamani na ya kisasa ni :
1 Alemanni- Ujerumani
2 Franks – Ufaransa
3 Anglo-Saxons- Uingereza
4 Burgudians - Uswizi
5 Visigoths –Uhispania
6 Suevi –Ureno
7 Lombards –Italia
8 Heruli
9 Vandals
10 OsyrogothsPembe Ndogo
Danieli 7:8. Nikazingalia sana pembe zake na tazama pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo milele. Mstari huu inatupa alama mbili inayo tuonyesha "pembe ndogo "katika Historia .
PEMBE NDOGO
( Nikaziangalia sana pembe zake na tazama pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.) Andiko hili linatupa mambo ya kuonyesha pembe ndogo katika historia. Kati ya zile pembe kumi (falme) na tatu kati ya zile za kwanza zilingolewa wakati ikianza kupokea nguvu. Baada ya zile kumi kuna ufalme mmoja tu katika historia yote inayo ambatana na maelezo hayo tuliyopewa. Katika ufalme wa Rumi, katikati yake wakati wa kuvunjika baada ya 476 A.D. UPAPA serikali ya mtu mmoja ya Kanisa ya Katoliki, wakati wa kuinuka kwake kabila za Gothic, Heruli, Vandals na Ostrgoths walingolewa na hawapatikani kamwe kwenye kumbukumbu ya historia. Utawala wa wafalme ukachukuliwa na Upapa utawala wa kipapa ulitangazwa rasmi na Justinian mwaka 533A.D na ukatekelezwa kwa nguvu za kijeshi mwaka wa 538 A.D kwa kuangusha kwa Ostrogoths na jenerali Belirarius wa mfalme Justinian.DHIBITISHO YA KUTAMATISHA
Mambo mengi zaidi yamo katika Danieli 7:25 " Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu naye ataazimu kubadili maneno ya sheria nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati na nyakati mbili na nusu wakati. Hii ni kuonyesha mateso makuu hakuna msomaji wa historia atakaye pingana na jukumu la kipapa kwa jambo hilo. Mateso ya kuogofya za giza yamo katika kumbukumbu za historia.
Naye ataazimu kubadili sheria jambo hili upapa kwa kuondoa amri ya pili inayokataza ibada ya sanamu na kubadilisha amri ya nne( ile inayoelezea wakati) siku ya uongo ya ibada imewekwa na Sabato ya siku ya saba ambayo Kristo na mitume waliabudu kuondolewa.
MIAKA 1260
Ishara nyingine inatisha bila shaka kwamba hakuna ufalme mwingine unaweza kulingana kwa maelezo hayo nayo ni kwamba atatawala miaka 1260. Hili limezungumzwa na Danieli mara mbili ufunuo mara tano kama ifuatavyo wakati na nyakati mbili na nusu wakati. Wakati= mwaka mmoja ( mwaka mmoja katika biblia ni siku 360 Nyakati mbili= miaka miwili (siku720) Danieli 7:25 na ufunuo 12:14 miezi arobaini na mbili ufunuo 11:2,13:5 na siku elfu na mia mbili na sitini Ufunuo 11:3 na 12:6 kalenda ya kinabii ya siku 360 ama miezi 12 ya siku zao ndiyo inayotumia katika bibilia.
Ufalme huu unatawala siku 1260 kila siku kwa mwaka ama miaka 1260 (Ezekieli 4: 6,Hesabu 14:34) kutoka mwaka 538 A.D wakati pembe ya mwisho kungolewa hadi 1798. Katika mwaka huo Berthier Generali wa Napoleons alifika na jeshi la Kifaransa Rumi na kumteka askofu wa Rumi Papa Pius VI mateka na kumpeleka Ufaransa alikoagia dunia nguvu za Kipapa zikimalizika na nchi Rumi kuwekwa.
Miaka 1260
538 A.D <-----------------------------------------> 1798 A.DLakini unabii wa kipapa haukuishia pale. Angalia maelezo zaidiya Ufunuo. Kwanza sura ya 13 tunapata mstari wa 1 hadi 10 inaeleza tena habari ya upapa ukainuka katika Ufalme wa Rumi iliyogawanyika nguvu zake wakati wa miaka 1260 jeraha la mauti iliyopata mwisho wa mwaka hiyo. Mstari wa tatu unasema Ufunuo 13:3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti na pigo lake la mauti likapona.
Tunaona katika Danieli 7:21,22 kwamba ufalme huu utakuwapo hadi wakati wa kuja kwa Kristo. Sasa tunaweza kuonyesha wazi mnyama wa Ufunuo 13:14-18 kama ni nini?
MNYAMA MWENYE PEMBE MFANO WA MWANA KONDOO NDIYE SANAMU YA MNYAMA.
Kati ya jeraha la mauti na kuinuka tena kuna mnyama mwingine anayeelezewa katika ufunuo 13:11,12 Mnyama huyu kutoka katika nchi ni taifa linalotokea katika nchi isiyokaliwa na watu.Ni taifa linalogunduliwa siyo kutekwa. Lina pembe mbili mfano wa mwana kondoo. Hii inaashiria uchanga unyenyekevu na kuwakilisha nguvu za kiserikali na kidini. Lakini alinena kama joka naye atumia uwezo wote wa mnyama wa kwanza naye afanya dunia yote wakao huko wamsujudie mnyama wa kwanza. Ni taifa moja katika historia inalingana na maelezo haya nalo ni umoja nchi za America( U.S.A) Tunaona katika msitari wa 14 kwamba ilianza kwa unyenyekevu lakini inabadilika baadaye.
Tunaona ikifanya sanamu ya yule mnyama wa kwanza mfano kamili ya upapa iliyokuwa wakati wa utawala wake wa 1260 wakati makanisa ya umoja wan chi ya America watakapo ungana kwa mafundisho yatakayowaleta pamoja. Watakapoungana na serikali ili kulazimisha kuitisha kwa sheria ili kutunza sheria zao.
Hapo ndipo America ya Kiprotestanti itakapotengeneza sanamu ya Utawala wa Kirumi .na adhabu ya Kiserikali kwa wale watakao kataaa itakuwa kuu..
Unabii unaonyesha kwamba America itakubali ibada ya siku ya Jumapili ambayo ndiyo alama ya mamlaka ya Kipapa kuunda sheria zake, na dunia yote itafuata. Ni kiburi cha Upapa kudai kubadilisha sheria za Mungu, amri kumi.Hii ndiyo itakayokuwa jambo la kuamua siku za mbele hata kuleta kifo ( ufunuo 13:14:15) sheria ya Mungu au sheria za wanadamu.
Kumbuka ya kwamba "naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni juu ya nchi mbele ya macho ya wanadamu". " wapate kuwapoteza kama yamkini wote walio wateule" Ufunuo 13:13 na Mathayo 24:24.
Upapa unadai kwamba kubalisha Sabato hadi siku ya kwanza Juma ni ishara ya nguvu na alama ya mamlaka yake katika mambo ya kidini .
Swali: Je mnayo njia nyingine ya kudhibitisha kuwa Kanisa lina mamlaka ya kubalisha maandiko?
Jibu: Tusingalikuwa na mamlaka, hatungeweza kubalisha jambo ambalo lina kubalika na madhehebu ya kuweka siku ya jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya Juma, badala ya Jumamosi iliyo siku ya saba, badiliko ambalo hakuna mamlaka ya maandiko.
(Katekismu ya mafundisho na Rev. Stephane Kenman, P. 174)
Kwa kweli Kanisa la Kikatoliki linadai kubalisha, na kubadilisha huku ni ishara ya mamlaka yake kwa mambo ya kidini.
Ikiwa Waprotestanti wangefuata Biblia, wangemwabudu Mungu siku ya Sabato. Kwa kuitii Jumapili, wanafuata sheria ya Kanisa Katoliki.
( Albert Smith, Chancellor wa Dayosisi ya Bathmore akajibu Kadinali kwa barua ya tarehe 10 Februari 1920)
ALAMA YA WANYAMA
Siyo tu alama ya nje ya kuonekana- Ingelikuwa hivyo ingelilazimishwa wote wanao pinga pekee. Wale wanaokataa alama ya mnyama ni wale wazishikazo amri za Mungu na imani ya Yesu ( Ufunuo 14:12) kwa hiyo wale walio na alama hii hawaitii sheria. Wale wanaopotea muhuri wa Mungu wanaushindi dhidi ya alama ya Mnyama ( Ufunuo 9:4,15:2) kwa hiyo alama ni kwa wale wavunjao sheria yake ( ama hapa chini)
Amri ya nne ambayo Rumi imejaribu kuondoa, ndiyo amri pekee inayoonyesha Mungu kama muumba , wa mbingu na nchi na hivyo kutofautisha Mungu wa kweli na miungu ya uongo. Sabato iliwekwa ili kuwa kumbukumbu ya uumbaji na hivyo kuelekeza mawazo ya mwanadamu kwa Mungu wa kweli aliye hai. Hakika ya nguvu za uumbaji wake zaonekana katika maandiko yote kama dhibitisho ya kuwa Mungu wa Israeli ni mkuu kuliko miungu yote ya mataifa. Kama Sabato ingelitiiwa mawazo ya mwanadamu na upendo wake ungelielekezwa kwa muumba wake, kama mwenye kuogopewa na kuabudiwa na kamwe hakungekuwa na waabudu sanamu, wasiomini wala washenzi.
Amri inayoonyesha Mungu kuwa ndiye Muumba ndiyo ishara ya mamlaka yake kwa viumbe alivyoumba. Kubalisha Sabato ndiyo ishara alama ya mamalaka ya Kanisa la Kirumi. Wale wanaotambua amri ya nne na kuchagua kuitii sabato ya Uongo badala ya Sabato ya kweli waonyesha utiifu kwa nguvu zilizo amrisha sheria hiyo.
Alama ya mnyama itakapowekwa katika kipaji cha uso ama mkononi kipaji cha uso inamaanisha kuamini mkononi ni kushirikiana na wenye mamlaka. Hakuna aliye na alama ya Mnyama leo. Itapokelewa tu wakati sheria ya kumataifa ya Jumapili iakapo lazimishwa na serikali ili kulazimisha dhamiri za watu wake na watoto kuambatana na uhuru wa kuabudu. Lakini wakati uabuduaji wa Jumapili itakapomalizimishwa kwa sheria dunia itaangaziwa kuhusiana na ibada ya sabato ya kweli isiyo na mamlaka ya juu ila ya kirumi watakuwa wakitii upapa badala ya Mungu. Amekubaliana na Rumi na mamlaka inayolazimisha sheria ya Kirumi. Anaabudu mnyama na sanamu yake. Wakati watu wanakataa maagizo ambayo Mungu ameweka kuwa ishara ya mamlaka yake, na badala yake kutii ile ambayo Rumi imechagua kama ishara ya mamlaka yake, watakuwa sasa wanakubali ishara ya uaminifu kwa Rumi- "alama ya mnyama" Ni mpaka wakati ambao watu watakuwa wamehubiriwa ukweli, ndipo sasa watakakuwa kuchagua amri za Mungu ama sheria za mwanadamu ndipo sasa wale watakao endelea kuasi watapokea "alama ya mnyama"
MUHURI WA MUNGU
ISHARA AMA MUHURI IMETUMIKA KATIKA BIBILIA KWA MAANA SAWA KUAMBATANA NA MAMBO MATATU.
Tazama: Muhuri wa kweli ni lazima uonyeshe vitu vitatu:-
- Jina la mwenye mamlaka
- Cheo chake au haki yake ya utawala
- Mahali anapo tawala au milki anayotawala
Kwa mfano
- Jina la mtu – Abraham Lincoln
- Cheo chake – Rais
- Milki yake – Umoja wa nchi za America (U.S.A)
Muhuri wa Mungu Unapatikana katika sheria zake na inapatikana katika amri ya nne
( Kutoka 20:8-11); " Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mnyama wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa."
Soma sheria zote kumi. Ni katika sheria ya nne ndio tunapata:-
- Jina la Mungu- Bwana Mungu Wako
- Cheo Chake- Muumba
- Milki Yake- Mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo.
Ezekiel aonyesha Sabato kuwa ishara ya Mungu ( Muhuri) (" andika Ezekiel 20:12") na Isaya 8:16.
Yesu alisema " Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Mtu mmoja alimjia Yesu na kuuliza Matayo 19:16-19 "Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Hapo mwanzo kulikuwapo Neno, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa baba, amejaa neema na kweli. Yohana 1:1-3,14 Sabato ya siku ya saba ni sheria moja katika sheria kumi za Mungu kumbusha la kila Juma kuwa Kristo ndiye muumbaji wetu na mkombozi.
Kanisa la masalio katika siku za mwisho wanashika sheria zote za Mungu Ufunuo 12:17 " Joka akamkasirikia yule mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.( mwanamke anawakilisha kanisa)
666
HESABU YA JINA LAKEUfunuo 13:18 “ Hapo ndipo hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. Kama mnyama ameelezewa, hesabu ya jina lake, bila ya kujali jinsi inavyoeleweka, lazima iwe na uhusiano na mamlaka haya. Hesabu kama vile unabii unasema, ni hesabu ya kibinadamu na kama inapatikana katika jina ama cheo,mwisho wake ni lazima iwe ni jina ama cheo cha mtu Fulani. Vicarius Filii Dei ikamaanisha "aliyekalia kiti cha mwana wa Mungu" ni moja wapo wa jina la papa wa kirumi aliyepia mpinga Kristo. Jumla ya hesabu ya silabi za jina ni 666 kama ifuatavyo.
V =
5
F =
0
D =
500
112
I =
1
I =
1
E =
0
53
C =
100
L =
50
I =
1
+ 501
A =
0
I =
1
=
501
= 666
R =
0
I =
1
I =
1
=
53
U* =
5
S =
0
=
112
(* U na V hubadilishana - angalia kwenye encyclopedia.)
Hapa kwa kweli tuna hesabu ya mtu Fulani ambaye ni mtu wa kuasi" na ni mtu mmoja na ya kwamba yampata achague jina la cheo chake ambalo linakufuru kama tabia mojawapo ya mnyama kisha jina hilo liandikwe kwenye vazi lake Rasmi kama kwa ajipandika hesabu ya 666. Siyo mapapa wote huvalia vazi lililo na jina la cheo, lakini kutokuvalia vazi hili halibadilishi chochote, kwa sababu Papa wote huwa " wanawakilishi wa Kristo" na majina ya kilatini yaliyo hapo juu ndio yanayodhihirisha cheo hiki hivi “ aliyekalia kiti cha kristo na jumla ya hesabu ni 666.
UJUMBE WA MALAIKA WATATU
Kuandaa watu wa Mungu ili kusimama katika siku ya Mungu, kazi kubwa ya matangenezo itamalizika. Mungu aliwezakuona kwamba watu wengi hawakuwa tayari kwa maisha milele. Kwa huruma zake aliekuwa tayari kutuma jumbe wa onyo ili kuwaamsha kutoka usingizi na kuwaongoza kujiandaa kwa kurudi kwa Bwana.
Onyo hili linapatikana katika kitabu cha Ufunuo 14. Hapa kuna jumbe hata zinazotangaza na malaika wa mbinguni na punde kufuatiwa na kurudi kwa mwana wa adamu kuvuna mavuno ya dunia.
UJUMBE WA MALAIKA WA KWANZA
Ujumbe wa kwanza wa onyo unatangazwa hukumu inakuja.
"Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu mwenye injili ya milele, awahubiri hao hao wakaao juu ya nchi na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu " Mcheni mungu na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja, msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji. Ufunuo 14: 6-7
Kutangazwa " saa ya hukumu inakuja" Inaashiria kukamilika kwa kazi ya upatinisho wa kristo kwa wokovu war oho. Inatangaza kweli ambayo itatangazwa hadi upatinishi wa mwokozi utakapokamilika na kisha arudi duniani kuwachukua walio wake. Kazi ya hukumu iliyoanza 1844 itaendelea hadi hukumu ya wote ikamilike. Wote walio hai na wafu kwa hiyo itaendelea hadi mwisho wa rehema. Ili watu wawe tayari kwa hukumu ujumbe huu unasema " Mche Mungu na kumtukuza" na umwabudu yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji. Matokeo ya kuukumbali ujumbe huu yaonyeshwa kuwa maneno haya " hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu" Ilikuweza kuwa tayari kwa hukumu ni lazima watu washike sheria za Mungu. Sheria hiyo ndiyo itakayo hukumu ni lazima watu washike sheria za Mungu. Sheria hiyo ndiyo itakuwa hukumu kila mmoja wetu. Mtume Paulo asema" " …………. Wote waliokosa wenye sheria watahukumiwa kwa sheria ……… katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu ….. kwa Kristo Yesu" Warumi 2: 12-16 Imani ni muhimu katka kutii sheria za Mungu; kwa kuwa "pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu" na "kila tendo lisilitoka katika imani ni dhambi" Waebrania 11: 6 ; Warumi 14:23
Malaika wa kwanza anawafanya watu "kumcha Mungu na kumtukuza" na kumwabudu kama muumba wa mbingu na nchi ;ili kufanya hivi lazima waitii sheria yake kama asemavyo muhubiri " Mche Mungu na uzishike sheria zake hakuna ibada inaweza kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake" waraka wa kwanza wa Johana 5:3, Methali 28:9
UJUMBE WA MALAIKA WA PILI.
Malaika wa kwanza afuatiwa na wapili akisema Ufunuo 14:8 " Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa" Neno hili babeli lamaanisha mchafuko imetumika katika maandiko kuonyesha madhehebu tofauti za uongo ama dini zilizo asi.
Ujumbe wa ufunuo 14 unaotangaza kuanguka kwa Babeli ni lazima iashirie kwa kuwa ujumbe huu unafata uwe wa lakini sasa yamenajisika kwa kuwa ujumbe huu unafuta ule wa hukumu, lazima itangazwe siku za mwisho, kwa hiyo haishiri kanisa la Kirumi pekee, kwa kuwa kanisa hilo limekuwa katika hali ya kuanguka karne nyingi zilizopita zaidi katika ufunuo 18 watu wa Mungu wanaitwa kutoka Babeli, kulingana na andiko hili watu wengi wa Mungu wanaitwa kutoka Babeli. Kulingana na andiko hili watu wengi wa Mungu wamo katika Babeli. Na ni katika madhehebu gani ndipo watu wengi walio wafuasi wa kristo wanapatikana. Bila ya shaka, ni madhehebu yanayodai kuwa na imani ya kiprotestanti.
Makanisa mengi ya kiprotestant yanafuata mfano wa rumi kwa kosa la kujishikanisha na " wafalme wanchi" Makanisa kwa ushirikiano na serikali na madhehebu mengine kwa kupata sifa za dunia, Babeli ( mchafuko) yawezekana kutumika kuashiria madhehebu kama hayo yanayo dai kuwa mafundisho ya bibilia. Mafundisho kutoka kwenye hali zimegawanyika makundi yaliyotofautiana kwa mafundisho na elimu.
Kado na kushirikiana na dhambi za ulimwengu makanisa yaliyojitenga kutoka rumi yanaendeleza tabia ya mafundisho yake.
- Ibada za sanamu kupitia kwa watakatifu na mafundisho yao.
- Ibada ya kutakasa siku ya Jumapili
- Kutokufa kwa nafsi
- Moto wa milele
- Wenye haki kwenda mbunguni
- Kukataa kuwa Kristo alikuweko hata kabla ya kuzaliwa Bethlehemu.
UJUMBE WA MALAIKA WA TATU
Ufunuo 14 9-12 Na mwingine mlaika wa tatu akawafuata akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, Yeye naye atakunywa katika mvinyo wa gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele za Mwana Kondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku hao wamsujudio huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeae chapa ya jina lake. Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.
Hapa tunasoma kwamba mtu yeyote aabuduye mnyama- Kanisa la Kirumi- na sanamu yake makanisa ya Kiprotestanti yanayoshirikiana na serikali kupitisha sheria za kidini, na kupokea chapa yake ibada ya Jumapili inayolazimika kwa sheria katika kipaji cha uso anayeamini kuwa ni kweli ama kwenye mkono wake wakuume kushirikiana na wenye mamlaka ili kuepuka adhabu watakunywa mvinyo wa ghadhabu ya wenye iliyotengezwa pasipo kuchanganywa na maji wataadhibiwa na Mungu katika moto amabo utawateketeza wote kabisa kiasi cha kusahaulika na wale watakaookolewa.
Onyo kali na la kuogofya kwa wanadamu ni ile ya ujumbe wa malaika wa tatu. Hii lazima iwe ni dhambi mbaya sana inayoleta hasira ya Mungu isiyo na huruma. Watu hawataachwa gizani kuhusiana na jambo hili lenye umuhimu onyo kuhusu dhambi hii itatolewa kwa ulimwengu wote kabla ya hukumu ya Mungu kuja, ile itatolewa kwa ulimwengu wote kabla ya hukumu ya Mungu kuja, ili wote wajue ni kwa nini wataadhirika na wapate njia ya kuepuka adhabu hiyo Unabii unasema kwamba malaika wa kwanza anatangazia " Kila taifa, na lugha, kabila na jamii" Onyo la malaika wa tatu ambayo ni mojawapo jumbe tatu kuu itahubiriwa kote katika unabii inaelezwa kwa sauti kuu na malaika anayeruka katikati ya mbingu na huyo itawatahadharisha walimwengu wote.
UJUMBE MALAIKA WA NNE
Baada ya hayo naliona malaika mwinginwe akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake, akalia kwa sauti kuu akisema Umeanguka uemanguka Baberi ule mkuu umekuwa maskani ya mashetani na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya gadhabu ya uasherati wake na wafalme wan chi wamezini naye na wafanya biashara wa nichi wamepata mali kwa nguvu za kiburi. Kasha nikaskia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhabi zake, wala msipokee mapigo yake, kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. Mlipeni kama yeye alivyowalipa, mkalipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake, katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara dufu. Ufunuo 18:1-6
Ufunuo 18 unaonyesha wakati ambapo, kutokana na kuukataa ujumbe wa onyo wa malaika 3 wa ufunuo 14:6-12 Kanisa litakuwa limefika hali ambayo tunaelezewa na malaika wa pili na watu wa Mungu walioko Babeli wataitwa kujitenga na ushirikiano wake, ujumbe huu ndio wa mwisho kupewa ulimwengu nao utakamilisha kazi yake. Wakati wale wote ambao hawakuamini kweli bali walikuwa wakijifurahisha katika udhadimu" ( Wathesalonike wa pili 2:12) wataachwa ili wapokee ule udanganyifu na kuamini uongo, kisha nuru itawaangazia wale wote ambao mioyo yao iloyo tayari kupokea, na ya kweli watu wote wa Mungu walio Babeli watasikia mwito " tokeni kwake enyi watu wengi" ( ufunuo 18:4)
Kwa kusoma yaliyo hapo juu, tataweza kuona yanayo maanishwa na Ujumbe Wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14.
- Inatatuambia yakuwa hukumu inaendelea sasa (mstari wa 6,7)
- Inatueleza kwamba Uprotestanti umaanguka kwa mujibu ya hii ,Ufunuo 18-5 inatuambia imekuwa ngome ya mashetani and kila Roho chafu .Tunaitwa tutoke katika mpangilio wa uongo wa kidini aina hii .
- Ujumbe wa kipekee unapewa ulimwengu ,ya kwamba mtu yeyote atakaye shuhudu Upapa au sanamu yake(yaani Uprotestanti na Serikali kuungana kulazimisha maagizo ya kibinadamu )na inaandamana na uabudu wa Jumapili watapokea alama ya mnyama.(mstari wa 9-11)
Mstari wa 12 unatuonyesha wale ambao hawakuipokea alama ya Mnyama ,lakini wanaitwa wenye kushika amri ya Mungu na ushuhuda wa Kristo(ikihusisha sabato ya siku ya saba).
Unaweza kuepuka?
Tukijua vile mambo yalivyo ,tunaweza kustaajabu kama inawezekana kutii Mungu na kuepuka hukumu yake ,tukijua haswa tumekuwa na maisha ya kutenda dhambi .Na dhambi ni nini ? "Kwani dhambi ni uasi (kuvunja)wa sheria" 1Yohana 3:4 na "mshahara wa dhambi ni mauti " Warumi 6:23 .Ni taraja gani tuliyo nayo?Hakuna ndani yetu ,"Je Mkushi aweza kuibadili ngozi yake au chui madoa-doa yake?,kama aweza ,ndipo na ninyi mliozoea kutenda mabaya ." Yeremia 13:23
Kalvari inakaa kama kumbusho ya kafara iliyohitajika kwa uvunjaji wa sheria ya Kiuungu Tusichukulie dhambi kama jambo ndogo .
Je mtu atakuwaja katika hali ya usawa na Mungu?
Je mwenya dhambi atafanyweje awe mwenye haki ?Ni kupitia tu Kristo ndipo tutakubalika na Mungu ,na kuwa wenye utakatifu ;lakini tutakujaje kwa Kristo?Wengi wanauliza swali sawa lililo ulizwa na umati siku ya Pentekoste , walipodhibitishiwa dhambi zao ,walilia "Tutafanya nini ?".Maneno ya kwanza ya Petero yalikuwa "Tubuni ".Matendo ya Mitume 2:37 ,38.Katika wakati mwingine,muda mfupi baadaye ,alisem "Tubuni ,mrejee,ili dhambi zenu zifutwe,zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuweko kwake Bwana ;
"Basi ,kwa kuwa watoto wenu wameshiriki damu na mwili ,yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo ,ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti ,yaani Ibilisi ,awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa .......Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa ,aweza kwasaidia wao wanaojaribiwa." Waebrania 2:14,15 18.
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu .Wafilipi 4:13.Tunaweza kudai nguvu hii tu tunapoikubali Haki yake kwa imani na kutubu .Kukiri na kuacha kutenda dhambi (yaani kuacha kuvunja sheria ya Mungu )na kumfuata yeye katika kutii.Lakini unaona rafiki ,imani na kutubu ni kipawa kutoka kwa Mungu (Warumi 12:3,2; 2Timotheo 2:25 )Kama katika jambo lolote,nasiyo kwa kitu unachoweza kujitengenezea mwenyewe ,tukijua hali yetu ,Yesu anasema kwetu “Ombeni ,nanyi mtapewa ;tafuteni ,nanyi mtaona;bisheni ,nanyi mtafunguliwa .....Basi ikiwa ninyi, mlio waovu ,mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema ,je si zaidi sana baba yenu aliye mbiguni atawapa mema wao wamuabuduo?.Mathayo 7:7,11.Kwa hivyo uliza Sasa kekama vile Daudi alifanya.
"Ee Mungu ,uniumbie moyo safi ,uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu .Usinitenge na uso wako .Wala roho yako mtakatifu isiniondolee.Unirudihie furaha ya wokovu wako ;uniegemeze kwa roho ya wepesi Zaburi 51-10-12 .Ni katika tu kumtegemea Kristo Yesu mia kwa mia amabye ni Mwokozi Aishiye ndipo tunaweza kuufikilia tabia kama- ya Kristo na kuwa tayari kukutana na mwokozi atakapo rudi ."Hili ni agano nitakaloagana naobaada ya siku zile, anena Bwana Nitatia sheria zangu mioyoni mwao ,na katika nia zao nitaziandika ,Waebrania10:16
Punde tu kabla ya Kristo kurudi hapa duniani ile sheria takatifu; haki ya Mungu iliyotangazwa kwa ngurumo na moto katika Sinai kama mwongozo wa maisha; sasa inadhihirishiwa kwa wanadamu kama sheria ya hukumu. Mkono utaonekana ukizifunguwa zile mbao mbili na hapo zitaonekana zile sheria za Mungu; zimeandika kana kwamba ni kalamu ya moto. Ni vigumu kuelezea uoga na wasiwasi wa wale waliyokanyagia sheria za Mungu chini.
Maadui wa sheria za Mungu; kutokea wachungaji hadi wale walio wadogo wao, sasa wanaiona ukweli na jukumu lake. Wakiwa wamechelewa
KWA KUTAMATISHA
Wataona ya kuwa Sabato ya Mungu katika sheria ya nne ndio muhuri wa Mungu aliye hali wakawa wakiwa wamechelewa wataona ukweli wa sabato ya uongo na msingi wa mchanga ambao wamekuwa wakijenga juu yake .Wakatambua ya kwamba wamekuwa wakiga vita dhidi yaMungu. Waalimu wa kidini wameongoza roho za watu kuangamia huku wakidai kuwaongoza hadi milango ya mbinguni. Ni mpaka tu siku ya mwisho ndipo tu itakapojulikana jukumu la uongozi na jinsi ilivyo ya kuongofya matokeo ya kutokuwa waaminifu ni katika umilele ndiyo twaweza kuona udhama wa nafsi iliyopokea itakuwa huzuni kwa wale ambao mungu atawaambia " ondokeni enyi watumishi waovu katika pambano kuu ulimwengu wa Kikristo utagawanyika makundi mawili makubwa wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale waabuduo mnyama na sanamu yake na kupokea chapa ya alama yake. Ingawa Kanisa na serikali zitaungana ili kulazimisha wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa. ( Ufunuo 13:16) Kuipokea" chapa ya mnyama" hali watu wa Mungu hawatapokea. Nabii Yohana akiwa Patmos alitizama " Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kiooo iliyochangamana na moto na wale wenye kushida, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando kando ya bahari hiyo wenye vinubi nvya Mungu. Nao wauimba wimbo wa musa mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo Ufunuo 15:2,3
Kumbuka hapo katika shamba la Edeni kutii kulijaribiwa katika miti miwili katika siku hizi za mwisho KUTII kutajibiwa na sheria za nani tunazoshika. Amri za Mungu ama sheria za wanadamu. Sabato ya Mungu au Jumapili ya kishenzi ulio mfano wake
Ufunuo 14:12
"Hapa ndipo penya subira ya Watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na Imani ya Yesu "
© D & S Goeldner, 1999.
Translation © by Philip Chegue, 2008.
![]()
BIBLICAL ARTEFACTS AND STUDIES
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |